HAPATOSHI 4 BORA REAL KIDS, FC MUEMBE BENI, SCHALKE 04 NA KING BOYS NANI BINGWA WA CENTRAL WILAYA YA MJINI MWAKA HUU?
![]() |
Kikosi cha Real Kids |
Na: Mosi Abdallah, Zanzibar.
Hatua ya nne bora ligi za madaraja ya Vijana ndani ya Wilaya
ya Mjini kwa upande wa daraja la Central inatarajiwa kuanza Jumamosi July 8,
2017 kwenye dimba la Amaan.
Akizungumza na Mtandao huu msemaji wa kamati ya Central
Wilaya hiyo Mussa Habibu “Mzirai” amesema tayari timu 4 zimeshapatikana ambazo
ni bingwa mtetezi FC Muembe beni, Real Kids, Schalke 04 na King Boys huku
mchezo wa kwanza utapigwa kati ya King Boys dhidi ya Muembe beni saa 4:00 za
asubuhi.
Amesema mchezo wa pili utapigwa Jumapili July 9, 2017 saa
4:00 za asubuhi kati ya Real Kids dhidi ya Schalke 04.
Kwa hatua nyengine Mzirai ameviomba vilabu hivyo kujiandaa
vizuri katika hatua hiyo kwani ni ngumu sana na kila timu itapata matokeo
kutokana na uwezo wao kwani kamati imejipanga kuhakikisha ligi hiyo inakuwa
bora.
“Sisi kama kamati tumejipanga ili ligi iwe bora na kuvuta
hisia za mashabiki kwani huku ndiko kunakotoka vipaji”. Alisema Mzirai.
Pia Mzirai ameziomba Kampuni, Mashirika ya UMMA na watu
binafsi kujitokeza kuidhamini ligi hiyo kwa kuwapa zawadi na wao wapo tayari
kufanya biashara na Kampuni yoyote kwani mpaka sasa hawajajua zawadi za
washindi wa Mashindano hayo.
Comments
Post a Comment