HATUCHEZI LIGI TWO KWASABABU SISI TUMEPANDA LIGI KUU ZANZIBAR-CHARAWE
Uongozi wa klabu ya Charawe Stars umefanya kikao chao kwa
Wanakijiji pamoja na Mashabiki wao wa Mjini kwa kauli moja wameamua kutocheza
ligi 2 na kutaka kupangiwa na ZFA kucheza ligi 1 ambayo ndio ligi kuu soka ya
Zanzibar kwa vile wao wamepanda daraja kucheza ligi hiyo.
Akizungumza na Mtandao huu Ramadhan Abdallah “Sadifa” ambae
ni msemaji mkuu wa timu hiyo amesema baada ya kumaliza kikao chao kwa pamoja
wameamua kususia kucheza ligi 2 ambayo ndio waliyopangiwa na msimamo wao ni
kucheza ligi 1 na sio ligi nyengine kwani wamepanda kucheza ligi kuu kwa nguvu
zao.
“Tumefanya kikao cha pamoja wadau wote wa timu ya Charawe wa
mjini na Kijijini na tumeamua kutocheza ligi 2, sisi msimamo wetu tucheze ligi
1 mana tumepanda daraja kwa nguvu zetu kisha leo tunaambiwa tucheze ligi 2,
hatukubaliani na uamuzi huo”. Alisema Sadifa.
Jumamosi ya July 8, 2017 Viongozi wa vilabu 28 vya Unguja na
Pemba walikutana katika ukumbi wa Uwanja wa Gombani kisiwani Pemba na kuamua
timu zitakazoshiriki ligi kuu soka ya kwa msimu wa mwaka 2017-2018 ambapo
wameamua timu zilizomaliza nafasi ya 1-6 kwa kila kanda, yani Unguja na Pemba
ndizo zitakazocheza ligi kuu wakati huo huo Bingwa atapata nafasi ya
kuwakilisha Zanzibar katika Kombe la Klabu Bingwa Barani Afrika.
Timu 16 kati ya 28 zilizosalia ambazo hazijashuka daraja
zitacheza ligi two ambapo Bingwa wa ligi hiyo atapata nafasi ya kuwakilisha
Zanzibar kwenye kombe la Shirikisho Barani Afrika.
Timu hizo 12 zilizofanikiwa kucheza ligi kuu (Ligi 1) msimu
mpya wa mwaka 2017-2018 ni JKU, Jang’ombe Boys, Zimamoto, Taifa ya Jang’ombe,
Polisi, KMKM kwa upande wa Unguja na Pemba ni Jamhuri, Kizimbani, Mwenge,
Okapi, Chipukizi na New Stars.
Kwa upande wa timu 16 zitakazocheza ligi 2 msimu mpya wa
mwaka 2017-2018 kati ya hizo 8 za Unguja na 8 za Pemba ambapo za Unguja ni Mafunzo,
KVZ, Black Sailors, Chuoni, Kilimani City, Kipanga, Miembeni City na Charawe
wakati za Pemba ni Dogomoro, Wawi Star, Shaba, Young Islander, FSC, Hardrock,
Chuo Basra na Opek ambapo timu 4 za mwisho za ligi 1 zitashuka daraja ligi 2,
na timu 4 za juu za ligi 2 zitapanda daraja la ligi 1 huku hoja yao kubwa
Charawe wao pamoja na Miembeni City, Chuo Basra na Opek wamesema walistahiki
kucheza ligi kuu kwa vile walipanda daraja lakini nafasi zao zikachukuliwa na
Polisi,KMKM, Chipukizi na New Stars waliyomaliza nafasi ya 5 na 6 kwa kanda ya
Unguja na Pemba kwenye ligi kuu msimu wa mwaka 2016-2017.
Comments
Post a Comment