HILIKA APIGA HATRICK ANGOZA KWA MABAO ZENJ
Ligi kuu soka ya Zanzibar hatua ya 8 bora imeendelea tena leo ambapo Zimamoto 4-1 Mwenge katika uwanja wa Gombani kisiwani Pemba.
Mshambuliaji wa Zimamoto Ibrahim Hamad Hilika amepiga hat rick katika dakika ya 24, 43 na 45 ambapo bao jengine limefungwa na Hassan Haji 30 huku bao pekee la Mwenge limefungwa na Abdull Yussuf dakika ya 88.
Kesho Jumanne ya July 18, 2017 mechi nyengine 3 ambapo Okapi watasukumana na Taifa ya Jang’ombe katika uwanja wa Gombani saa 10:00 za jioni, na katika uwanja wa Amaan JKU watakipiga na Kizimbani saa 10:00 za jioni, kisha saa 1:00 za usiku Jang'ombe boys dhidi ya Jamhuri.
Ikumbukwe kuwa hatua hiyo ya 8 bora ni kwaajili ya kuwatafuta Wawakilishi wa Zanzibar watakaoshiriki Mashindano ya Kimataifa ambapo Bingwa atawakilisha kwenye Kombe la Klabu Bingwa Barani Afrika na mshindi wa pili atawakilisha kwenye Kombe la Shirikisho Barani humo ambapo msimu uliopita Zimamoto na KVZ waliwakilisha Zanzibar katika Mashindano hayo.
Comments
Post a Comment