HILIKA AWATULIZA KIZIMBANI, JKU YAENDELEA KUTESA PEMBA, KESHO HAPATOSHI TAIFA NA JAMHURI
Ligi kuu soka ya Zanzibar hatua ya 8 bora imeendelea tena
jioni ya leo katika viwanja viwili tofauti.
Katika uwanja wa Amaan Zimamoto wamefanikiwa kupata ushindi
wa mabao 2-0 dhidi ya Kizimbani.
Mabao yote ya Zimamoto yamefungwa na Ibrahim Hamad Hilika
dakika ya 53 na 84.
Na katika uwanja wa Gombani kisiwani Pemba JKU imeendelea
kuwika baada ya kuwafunga Mwenge mabao 3-1.
Mabao ya JKU yamefungwa na Nassor Mattar dakika ya 26, Salum
Said Salum dakika ya 31 na Khamis Said Khamis dakika 44 huku bao pekee la
Mwenge limefungwa na Faki Shaibu dakika 83.
Ligi hiyo itaendelea kesho kwa kupigwa mchezo kati ya Taifa
ya Jang'ombe dhidi ya Jamhuri saa 10 za jioni katika uwanja wa Amaan, na katika uwanja wa Gombani Jang'ombe Boys
watasukumana na Okapi saa 10 za jioni.
Comments
Post a Comment