JAMHURI AZIZIMA SILAHA ZA ZIMAMOTO, YAENDELEA KUTESA ZANZIBAR
Kinara wa ligi kuu soka ya Zanzibar timu ya Jamhuri imeendelea kutamba baada ya jioni ya leo kuwafunga Zimamoto mabao 2-1 mchezo uliopigwa katika uwanja wa Amaan.
Mabao ya Jamhuri yamefungwa na Mussa Ali dakika ya 7 na Mohamed Ali dakika ya 17,huku bao la zimamoto limewekwa kimiani na Hassan Haji dakika 39.
Nako huko katika uwanja wa Gombani JKU wametamba mbele ya Okapi baada ya kushinda mabao 2-1.
Mabao ya JKU yamefungwa na Nassor Mattar dakika ya 10 na 34 wakati bao la Okapi likifungwa na Khamis Said dakika ya 70.
Ligi hiyo itaendelea tena Alhamis July 13, 2017 kati ya Zimamoto dhidi ya Kizimbani saa 10 za jioni katika uwanja wa Amaan, na katika dimba la Gombani watasukumana kati ya Mwenge dhidi ya JKU saa 10 za jioni.
Comments
Post a Comment