JKU ACADEMY NOWMA, YAWAPIGA WENZAO 5-0 MASHINDANO YA ROLLING STONE
Timu ya JKU Academy imetisha jioni ya leo katika Mashindano ya Vijana ya Afrika na Kati ya Rolling stone baada ya kuifunga Namanga Academy mabao 5-0 uwanja wa Mirerani Simanjiro.
Mabao ya JKU yamefungwa na Abdallah Salum (mawili), Salehe Mshamu, Hamid Bakar na Mudrik Ally.
JKU Academy watacheza tena kesho kutwa Jumatano July 12, 2017 saa 10 za jioni dhidi ya timu ya Middle H katika uwanja wa Mirerani.
Comments
Post a Comment