KESHO NDIO KESHO KUJUA MFUMO UPI WA KUPATIKANA TIMU 12 ZA LIGI KUU MSIMU MPYA 2017-2018 UTAJULIKANA
Baadhi ya wajumbe wa Vilabu vya Soka Unguja wamesafiri kwa
Meli ya MV Mapinduzi asubuhi ya leo kwenda kisiwani Pemba katika kikao maalum
cha Vilabu 28 ambavyo vimo katika
mchakato wa upatikanaji wa timu 12 za ligi kuu soka ya Zanzibar msimu mpya wa
mwaka 2017-2018 ambapo watakutana na kupanga mchakato mzima wa upatikanaji wa
timu kumi na mbili za ligi kuu msimu wa 2017-2018, kikao ambacho kitafanyika
kesho Jumamosi ya July 8, 2017 saa 3:00 za asubuhi katika Ukumbi wa Mikutano wa
uwanja wa Gombani Kisiwani Pemba.
Hayo yote yamekuja baada ya ZFA kuwa mwanachama wa 55 wa
Shirikisho la Soka Barani Afrika “CAF” ambapo moja ya agizo lao CAF ni kutaka
msimu ujao wa mwaka 2017-2018 ligi kuu soka ya Zanzibar iwe na jumla ya timu 12
kwa Zanzibar nzima ambapo katika msimu huo wa mwaka 2016-2017 ulikuwa na jumla
ya timu 36 kwa kila kanda ilikuwa ina timu 18, yani Kanda ya Unguja 18 na Kanda
ya Pemba 18, huku zimeshashuka timu 12 kati ya hizo 36 kwa kila kanda zimeshuka
timu sita (6).
Viongozi wawili wawili wa Timu 14 za Unguja wanaohitajika Pemba
katika Mkutano huo ni kutoka JKU, Zimamoto, Jang’ombe Boys, Taifa ya Jang’ombe,
Mafunzo, KMKM, Black Sailors, Polisi, Chuoni, Kipanga, Kilimani City,KVZ ,
Miembeni City na Charawe ambapo watashirikiana na vile vilabu 14 vya Pemba ili
kupanga mchakato mzima wa upatikanaji wa
timu kumi na mbili za ligi kuu msimu wa 2017-2018.
Comments
Post a Comment