KOCHA KIDUU MWENYE LESENI “A” LICHA YA KUONGOZA LIGI YA ZENJ BADO AKIRI KUWA NGUMU
Kocha Mkuu wa timu ya Jamhuri, Abdul mutik Haji (Kiduu),
amekiri ligi kuu ya Zanzibar hatua ya 8 bora ni ngumu na kwamba hadi sasa na hakuna
timu ambayo imejihakikishia kutwaa ubingwa wa ligi hiyo inayofikia tamati Jumapili
ya 20/8/2017.
Kiduu amesema licha ya timu yake kuongoza lakini bado ligi
mbichi na timu zote 8 zina nafasi lakini atapigana kuhakikisha timu yake
inaendelea kuongoza hadi mwisho wa ligi hiyo.
“Bado ligi ni ngumu mno, timu yoyote ina nafasi ya kutwaa
ubingwa, mimi kubwa ntahakikisha naendelea kuongoza mpaka mwisho”. Alisema
Kiduu.
Jamhuri ndie kinara wa ligi kuu soka ya Zanzibar hatua ya 8
bora akiwa na alama 12 akipata ushindi michezo yote 4 baada ya awali kuwafunga
Mwenge mabao 3-2, kisha kuwachapa Okapi 3-0, wakaendelea kuwapiga Kizimbani 3-0
na juzi tu wakawamaliza Zimamoto kwa mabao 2-1.
The great
ReplyDelete