FAINALI LEO KOMBAIN YA MJINI KUTETEA TAJI LAO DHIDI YA FIRE BOYS, MASHINDANO YA ROLLING STONE
Mabingwa watetezi wa Mashindano ya Vijana ya Afrika Mashariki
na Kati ya Rolling Stone timu ya Mjini Unguja leo watatetea taji lao kwa kucheza fainali
dhidi ya Fire Boys ya Karatu mchezo utapigwa saa 10:00 za jioni katika uwanja
wa Julious Nyerere huko Mbulu Mkoani Manyara.
Timu hizo zilikutana katika hatua ya makundi ambapo Mjini
Unguja iliwafunga Fire Boys mabao 2-0 kwa bao za Ibrahim Abdallah "Imu
Mkoko" na Abdul hamid Juma "Samatta".
Ikumbukwe
kuwa Mjini Unguja ndio mabingwa watetezi wa Mashindano hayo kombe ambalo
walilichukua tarehe 9 July, 2016 siku ya Jumamosi timu hiyo ya ilipotwaa ubingwa
huo wa Rolling stone kwa mara ya Kwanza ndani ya miaka 15 baada ya kuibuka na
ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya DAREDA ya Mkoani Manyara katika uwanja wa SHEIKH
AMRI ABEID mjini Arusha.
Mashindano ya Mpira wa Miguu kwa
Vijana waliochini ya umri wa miaka 17 Afrika Mashariki na Kati maarufu kama
Rolling Stone, Mwaka huu 2017 yanafanyika katika Mikoa Ya Arusha na Manyara
huku Manyara wakipata fursa ya Kuandaa Mashindano Hayo Kwa Mara ya Kwanza na
kupewa Vituo Vitatu Vya Mbulu,Babati na Mererani.
Comments
Post a Comment