KOMBAIN YA MJINI TENA NA DULLA BOYS KESHO, JUMATANO WATAKIPIGA NA KWEREKWE CITY
![]() |
Ali Juma "Mabata" mlinzi wa Mjini |
Timu ya Kombain ya Wilaya ya Mjini inatarajia kucheza mchezo
wa kirafiki na Dulla Boys kesho Jumatatu July 3, 2017 saa 10:00 za jioni katika
uwanja wa Amaan.
Kiingilio cha mchezo huo ni Shilingi Elfu moja na V.I.P ni
shilingi Elfu mbili.
Mchezo wa mwisho wa kirafiki Mjini watacheza na Kwerekwe City
siku ya Jumatano July 5, 2017 saa 10:00 za jioni katika uwanja wa Amaan.
Kombain ya Mjini wanajiandaa na Mashindano ya Rolling Stone
yanayotarajiwa kuanza July 9 hadi July 19, 2017 huko Mbulu Manyara.
Comments
Post a Comment