KOMBAIN YA MJINI WATINGA FAINALI KIRAHISI BAADA YA WAPINZANI WAO KUSHINDWA KUWAFATA, SASA WANAWASUBIRI NDUGU ZAO JKU FAINALI
Mabingwa watetezi wa Mashindano ya Vijana ya Afrika Mashariki
na Kati ya Rolling Stone timu ya Kombain ya Mjini Unguja imefanikiwa kutinga
hatua ya fainali baada ya wapinzani wao Saint Patrick Academy ya Arusha
kushindwa kusafiri kwenda Mbulu Mkoani Manyara wakitokea huko Arusha kucheza na
wapinzani wao Mjini mchezo ambao wa nusu fainali ulikuwa usukumwe kesho majira
ya saa 10 za jioni katika uwanja wa Julias Nyerere.
Akithibitisha taarifa hizo Mwenyekiti wa Mashindano hayo
Wilium Zongwe (Dell Piero) amesema Saint Patrick Academy wameshindwa kwenda
huko Mbulu kutokana na gharama za fedha hivyo Mjini Unguja wametinga wao moja
kwa moja fainali.
“Saint Patrick Academy washatoa taarifa kama hawatoweza
kufika Mbulu kesho katika mchezo wao wa nusu fainali dhidi ya Mjini kutokana na
uhaba wa fedha, hivyo Mjini wameshafanikiwa kufika fainali moja kwa moja”.
Lakini inasemekana kuwa timu ya Saint Patrick Academy ya
Arusha imewaogopa Mjini Unguja baada ya kutoa dozi nene hasa baada ya jana
kuwachapa Lindi academy kwa mabao 5-1 huku magoli ya Mjini yalifungwa na
Ibrahim Abdalla (Imu Mkoko ) 2, Mohamed Mussa (Modi) 2 na Mohamed Haji (X Box)
1, hivyo sababu ya kushindwa kumudu gharama ni kisingizio tu.
Kwa maamuzi hayo Mjini Unguja watasubiri kucheza fainali siku
ya Jumanne ya July 18, 2017 na mshindi wa nusu fainali ya pili kati ya JKU
Academy kutoka Zanzibar au Fire Boys kutoka Karatu Arusha.
Comments
Post a Comment