MAKAMO WA RAIS ZFA AFUNGUA KOZI YA MAKOCHA WA MAKIPA ZANZIBAR
Makamo wa Rais ZFA Unguja Mzee Zam Ali leo saa 3:00 za asubuhi
alikuwa Mgeni Rasmi katika ufunguzi wa Kozi
ya awali ya makocha wa Magilikipa, kozi ambayo imeanza leo Jumatano July 5 na kumalizika Jumanne July 11, 2017
chini ya Mkufunzi Gwiji Saleh Ahmed Seif
“Machupa”.
Kozi hiyo imeandaliwa na Chama cha Soka Zanzibar “ZFA” ambayo
itawashirikisha zaidi ya makocha 30 kutoka Unguja na Pemba na makocha hao
wakimaliza kozi hiyo watapata fursa ya kutambuliwa na Shirikisho la Soka Barani
Afrika “CAF”.
Machupa ni Mkufunzi pekee nchini Tanzania aliyehitimu Kozi ya
CAF ya Wakufunzi wa Makocha wa Magolikipa wa ndani kozi ambayo aliisomea nchini
Cameroon mwanzoni mwa mwezi Mei mwaka huu,
Machupa pia ameshahitimu kozi ya FIFA ya Ukocha wa Magolikipa ya hatua
ya juu (Advanced Level) ambayo aliipata kwenye kozi iliyofayika tarehe 01
Agost, 2016 na kumalizika tarehe 05 Agost 2016, na pia Machupa ana Leseni “B”
ya Ukocha inayotambuliwa na CAF.
Comments
Post a Comment