MAPINDUZI IMEWAPINDUA NEW POWER LIGI YA MABINGWA WILAYA
Timu ya Mapinduzi kutoka Wilaya ya Kusini Unguja imefanikiwa
kuondoka na alama 3 muhimu baada ya kuifunga 1-0 New Power kutoka Wilaya ya
Kati, kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa wa Daraja la Pili Wilaya pambano lililopigwa
leo saa10 za jioni katika Uwanja wa Amaan.
Bao pekee la Mapinduzi limefungwa na Ali Ameir dakika ya 77
ya mchezo huo.
Ligi hiyo itaendelea tena kama ratiba ilivyo hapo chini:-
11/7/017 Kianga Int vs Shingwi Heroes
12/7/017 African Boys vs Kwerekwe City
15/7/017 New King vs Super Tiger
16/7/017 Uhuru vs Nyangobo
Mechi zote hizo zitachezwa saa 10:00 alasiri uwanja wa Amaan
Comments
Post a Comment