MFUNGAJI WA JAMHURI KUKOSA MECHI ZOTE ZA JULY LIGI KUU YA ZANZIBAR
Mshambuliaji
hatari wa klabu ya Jamhuri Khamis Abdulrahman Hamad “Mburu” atalazimika kukaa
nje ya uwanja kwa kipindi cha wiki tatu.
Nyota huyo atakaa
nje ya uwanja kwa wiki tatu kufuatia kuchanika kwa nyama za paja la kushoto akiuguza
jeraha hilo ambapo atakosa zaidi ya michezo 8 katika ligi kuu soka ya Zanzibar
hatua ya 8 bora.
Mburu ataanza
kukosa michezo miwili yote timu yake itakayocheza Unguja katika Uwanja wa Amaan
ukiwemo wa Jumatatu July 10 kati ya Zimamoto dhidi ya Jamhuri, na mwengine wa
Alhamis July 13, 2017 kati ya Taifa ya Jang’ombe dhidi ya Jamhuri ambapo pia
akitarajiwa kukosa na michezo mengine ambayo yote itakayochezwa mwezi July.
“Daktari
amenambia nitakaa nje zaidi ya wiki 3, ila kwasasa naendelea vizuri afya yangu
namshkuru Mwenyezi Mungu, mana paja langu la kushoto lilichanika sana juzi”.
Alisema Mburu.
Mungu amfanyie wepesi nguli huyo
ReplyDelete