MJINI UNGUJA NA JKU CADEMY WAKISHINDA WOTE KESHO NUSU FAINALI, BASI WATAKUTANA FAINALI MASHINDANO YA ROLLING STONE
![]() |
Kikosi cha Mjini Unguja cha jana kilichoshinda 5-1 robo fainali |
Na: Kennedy Lucas na Said Salim “Hazard” kutoka Mbulu, Manyara.
Baada ya jana kushinda Wawakilishi wawili wote wa Zanzibar
katika Mashindano ya vijana ya Afrika Mashariki na kati ya Rolling Stone timu
ya Mjini Unguja na JKU Academy ambao wamefanikiwa kutinga hatua ya nusu
fainali, sasa kesho wakifanikiwa kushinda katika michezo yao ya nusu fainali
watakutana fainali Wazanzibar wawili hao.
Mjini Unguja jana walitinga nusu fainali baada ya kuitoa Lindi
academy kwa mabao 5-1 huku magoli ya Mjini yalifungwa na Ibrahim Abdalla (Imu Mkoko
)2, Mohamed Mussa (Modi) 2 na Mohamed Haji (X Box) 1.
JKU Academu wametinga hatua ya nusu fainali baada ya Arusha
Center Academy ya Arusha kuondolewa Kwenye Mashindano hayo baada ya
kuwachezesha wachezaji wanne ambao umri wao umezidi miaka 17 katika mchezo wao
wa Robo fainali ya Mashindano hayo dhidi ya JKU mchezo ulipigwa katika uwanja
wa kumbukumbu ya Sheikh Amri Abeid Kaluta Jijini Arusha Ambapo Arusha Center
waliibuka na ushindi wa bao 1-0.
Baada ya mchezo kumalizika JKU walikata rufaa wakiilalamikia
Arusha Center Kuwachezesha Wachezaji 3 ambao wanaumri zaidi Ya Miaka 17 ambayo
hairuhusiwi kutokana na kanuni na taratibu zinavyo sema kwani Mchezaji anaeruhusiwa
kucheza Mashindano hayo ni mwenye umri wa chini ya miaka 17.
Baada ya kuipitia rufaa hiyo Kamati Ya Mashindano ya Rolling
Stone ikaamua kuiondosha katika Mashindano hayo timu Ya Arusha Center Academy
kutokana na timu hiyo kuchezesha Wachezaji ambao hawaruhusiwi kucheza, hivyo JKU
Academy Sasa wamepita kwa Rufaa hiyo.
Mapema kesho Jumapili saa 8:00 za mchana JKU Academy kutoka Zanzibar
watasukumana na Fire Boys kutoka Karatu Arusha kwenye mchezo wa nusu fainali ya
kwanza.
Mabingwa watetezi timu ya Kombain ya Mjini kutoka Zanzibar
watacheza nusu fainali ya pili dhidi ya Trust Saint Patrick Academy ya Arusha
mchezo utapigwa saa 10:00 za jioni.
Michezo yote hiyo itapigwa katika uwanja wa Julias Nyerere Wilayani
Mbulu Mkoani Manyara.
Jumatatu ya July 7, 2017 ni siku ya mapumziko ambapo Jumanne
ya July 18, 2017 ni siku ya kutafuta Mshindi wa 3, 2 na Bingwa.
Mashindano ya Mpira wa Miguu kwa Vijana waliochini ya umri wa
miaka 17 Afrika Mashariki na Kati maarufu kama Rolling Stone, Mwaka huu 2017
yanafanyika katika Mikoa Ya Arusha na Manyara huku Manyara wakipata fursa ya Kuandaa
Mashindano Hayo Kwa Mara ya Kwanza na kupewa Vituo Vitatu Vya Mbulu,Babati na
Mererani wakati changamoto kubwa katika Mashindano hayo yakiwa ni uchezeshwaji
wa Wachezaji Wenye Umri Zaid Ya Miaka 17.
Comments
Post a Comment