MJINI UNGUJA WATWAA UBINGWA TENA ROLLING STONE
Timu ya Kombain ya Mjini Unguja imefanikiwa kutwaa tena ubingwa wa Mashindano ya Vijana ya Afrika Mashariki na Kati ya Rolling Stone baada ya kuwafunga timu ya Fire Boys kutoka Karatu mabao 2-0 fainali iliyopigwa jioni ya leo katika uwanja wa Julious Nyerere huko Mbulu Mkoani Manyara.
Mabao ya Mjini Unguja yamefungwa na Ibrahim Abdallah (Mkoko) na Seifu Said (Tiote).
Comments
Post a Comment