MJINI UNGUJA YATETEA TAJI LAO VYEMA, LEO YATINGA ROBO FAINALI ROLLING STONE
Mabingwa watetezi wa Mashindano ya Vijana ya Afrika Mashariki na Kati ya Rolling Stone timu ya Mjini Unguja imefanikiwa kutinga hatua ya robo fainali katika Mashindano hayo kufuatia kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Fire Boys ya Karatu mchezo uliosukumwa jioni ya leo katika uwanja wa Julious Nyerere huko Mbulu Mkoani Manyara.
Mabao ya Mjini yamefungwa na Ibrahim Abdallah "Imu Mkoko" na Abdul hamid Juma "Samatta".
Robo fainali Mjini wanatarajia kucheza Ijumaa ambapo bado hawajamjua mpinzani wao.
Comments
Post a Comment