MKUU WA MKOA WA MJINI MAGHARIBI AZINDUA KIPWIDA CUP
Mashindano ya Kipwida CUP yameanza rasmi jioni ya leo katika
uwanja wa Lion Kids kwa mchezo kati ya Kisakasaka United na Big Nation
uliomalizika kwa Kisakasaka kufungwa mabao 2-1, ambapo Mgeni Rasmi alikuwa Mkuu
wa Mkoa wa Mjini Magharibi Ayoub Mohammed Mahmoud.
Kisakasaka ndio waliotangulia kupata bao katika dakika ya 12
kupitia kwa Abdillah Ali na kusawazishiwa dakika ya 77 kupitia kwa Ramadhan
Yussuf ambae alifunga ena dakika ya 82.
Ligi hiyo inatarajiwa kuendelea tena kesho kwa mchezo mmoja
kati ya Basra Boys dhidi ya Mpira Pesa katika Uwanja wa Lion Kids saa 10 za
jioni.
Na: Mwajuma Juma, Zanzibar.
Comments
Post a Comment