MLANDEGE WAPANIA KUPANDA DARAJA, WAANZA KWA KISHINDO LEO
Timu ya Mlandege kutoka Wilaya ya Mjini imeanza vyema ligi ya mabingwa wa Daraja la Pili Wilaya baada ya jioni ya leo kuwafunga Azimio ya Wilaya ya Magharibi "B" mabao 3-0 mchezo uliosukumwa katika uwanja wa Amani.
Mabao ya Mlandege yamefungwa na Sajini Remtula dakika 15, Hassan Ramadhan dakika 31 na Omar Makame Makungu dakika ya 70.
Ligi hiyo itaendelea tena kesho kwa kupigwa mchezo mmoja katika uwanja wa Amaan kati ya Mapinduzi kutoka Wilaya ya Kusini watasukumana na New Power kutoka Wilaya ya Kati saa10 za jioni.
Comments
Post a Comment