NINJA WA ZANZIBAR AKIWA NA UZI WA YANGA
Mlinzi mpya wa Yanga Abdallah Haji Shaibu "Ninja"ni
miongoni mwa wachezaji wa Yanga waliyoanza mazoezi tangu Jumanne na kikosi chao
kwa kujiandaa na mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Simba pamoja na ligi kuu soka
Tanzania bara.
Ninja ndie mchezaji wa kwanza msimu huu wa mwaka 2017-2018 kusajiliwa
Yanga akitokea Taifa ya Jang’ombe ya Zanzibar ambapo amefunga mkataba wa miaka
miwili kuitumikia klabu hiyo.
Yanga ilianza mazoezi rasmi uwanjani tangu Jumanne ya July
11, 2017 na kuanzia Jumatano ya July 12, 2017 hadi leo asubuhi walifanya
mazoezi yao kwenye gym ili kujiweka sawa zaidi.
Comments
Post a Comment