RAIS WA JANG’OMMBE BOYS AONYESHA MAKALI YAKE MPAKA PEMBA, BOYS WAKIIPIGA MWENGE, BAADAE ZAMU YA TAIFA
Mshambuliaji hatari wa timu ya Soka ya Jang’ombe Boys Khamis
Mussa (Rais) ameendelea kuonyesha makali yake baada ya kufunga mabao yote
mawili timu yake ilipoichapa Mwenge mabao 2-1 katika mchezo wa ligi kuu soka ya
Zanzibar hatua ya 8 bora uliosukumwa jioni ya leo katika uwanja wa Gombani.
Rais mabao hayo ameyafunga katika dakika ya 27 na 77 ambapo Mwenge walitangulia kupata bao
lililofungwa na Ali Salim Bajaka dakika ya 18 ya mchezo huo.
Ligi hiyo itaendelea tena baadae saa 1 za usiku katika Uwanja
wa Amaan kati ya Taifa ya Jang’ombe dhidi ya Kizimbani.
RATIBA YA MECHI ZA
KESHO:-
10/7/017 Okapi vs JKU saa 10 alasiri uwanja wa Gombani
10/7/017 Zimamoto vs Jamhuri saa 10 alasiri uwanja wa Amaan
Comments
Post a Comment