RASMI VILABU 12 VYA LIGI KUU ZANZIBAR VIMEPATIKANA, SASA KUTAKUWA NA LIGI ONE NA TWO, MIEMBENI CITY NA CHARAWE HAWAMO LIGI KUU JAPO WAMEPANDA
Viongozi wa vilabu 28 vya Unguja na Pemba wamekutana leo katika
ukumbi wa Uwanja wa Gombani kisiwani Pemba na kuamua timu zitakazoshiriki ligi
kuu soka ya kwa msimu wa mwaka 2017-2018 ambapo wameamua timu zilizomaliza
nafasi ya 1-6 kwa kila kanda, yani Unguja na Pemba ndizo zitakazocheza ligi kuu
wakati huo huo Bingwa atapata nafasi ya kuwakilisha Zanzibar katika Kombe la
Klabu Bingwa Barani Afrika.
Timu 16 kati ya 28 zilizosalia ambazo hazijashuka daraja zitacheza
ligi two ambapo Bingwa wa ligi hiyo atapata nafasi ya kuwakilisha Zanzibar
kwenye kombe la Shirikisho Barani Afrika.
Timu hizo 12 zilizofanikiwa kucheza ligi kuu msimu mpya wa
mwaka 2017-2018 ni JKU, Jang’ombe Boys, Zimamoto, Taifa ya Jang’ombe, Polisi,
KMKM kwa upande wa Unguja na Pemba ni Jamhuri, Kizimbani, Mwenge, Okapi, Chipukizi
na New Stars.
Kwa upande wa timu 16 zitakazocheza ligi 2 msimu mpya wa
mwaka 2017-2018 kati ya hizo 8 za Unguja na 8 za Pemba ambapo za Unguja ni Mafunzo,
KVZ, Black Sailors, Chuoni, Kilimani City, Kipanga, Miembeni City na Charawe wakati
za Pemba ni Dogomoro, Wawi Star, Shaba, Young Islander, FSC, Hardrock, Chuo
Basra na Opek.
Timu 4 za mwisho za ligi 1 zitashuka daraja ligi 2, na timu 4
za juu za ligi 2 zitapanda daraja la ligi 1.
Comments
Post a Comment