SERIKALI YA ZANZIBAR YAZUNGUMZIA KUHUSU ZFA KUONDOSHWA CAF, WAOMBWA WAZANZIBAR KUWA WATULIVU, SASA WANASUBIRI TAARIFA RASMI KWA VIONGOZI WA ZFA WALIKUWEPO KWENYE MKUTANO WA SHIRIKISHO HILO
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Utalii Utamaduni na Michezo Zanzibar
Omar Hassan Omar “King” amewataka Wazanzibar kuwa wastahamilivu na kuwa na
subira katika kipindi hichi kigumu baada ya Zanzibar kuondolewa uanachama wao
wa 55 wa kudumu wa Shirikisho la Soka Barani Afrika “CAF”.
King amesema wanachosubiri sasa ni ujio wa viongozi wa ZFA
ambao waliokuwepo mjini Rabat, Morocco kwenye kikao cha Kamati utendaji ya CAF, viongozi ambao
walikuwemo kwenye kikao hicho ambacho kuliamua mambo kadhaa likiwemo hilo la
Zanzibar kufutiwa uanachama wake, na baada ya ripoti hiyo ya ZFA wao Serikali watatoa
taarifa rasmi.
Viongozi wa ZFA walikuwepo katika Mkutano huo ni Rais wa ZFA
Ravia Idarous Faina, Katibu Mkuu wa ZFA Mohd Ali Hilali “Tedy” pamoja na kocha
mkuu wa timu ya Taifa ya Zanzibar (Zanzibar Heroes) Hemed Suleiman “Morocco”
ambao wanatarajiwa kuwasili Visiwani Zanzibar kesho Jumatatu ya July 24, 2017
kwenye uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume kuanzia majira ya saa
2 za usiku.
“Kama mulivyosikia tumeondolewa uanachama na CAF, lakini
tunachokisubiri kwasasa ni kuweza kupata taarifa rasmi kutoka kwa ZFA na kupata
barua ambayo itawasilishwa ZFA baadae barua ile kuwasilishwa Serikalini na pale
ndipo tutaweza kujua ni ipi sababu gani ilipopelekea kutolewa, cha msingi jambo
hili limetusikitisha sana Wazanzibar lakini mimi naomba tuwe watulivu kisha
tuwe na subira katika kipindi hichi, baada ya hapo tutatoa taarifa rasmi kutoka
Serikalini”.Alisema King.
Juzi Rais wa CAF, Ahmad Ahman amesema Zanzibar ilipewa nafasi
hiyo kimakosa na si sahihi kwa nchi moja kuwa na wanachama wawili wa shirikisho
hilo.
Zanzibar ilipewa uanachama wakati wa utawala wa Issa Hayatou
ambaye alikuwa akiungwa mkono na TFF chini ya Jamal Malinzi, hata hivyo Hayatou
aliangushwa na Ahmad Ahmad ambaye aliibuka mshindi katika uchaguzi wa CAF
ambapo uanachama huo kwa Zanzibar ulidumu kwa siku 128 kuanzia Alhamis ya Machi 16, 2017 hadi juzi
Ijumaa ya July 21, 2017.
Comments
Post a Comment