SIKU 128 HAKIKA WAZANZIBAR WATAENDELEA KUZIKUMBUKA BAADA YA KUWA MWANACHAMA WA 55 WA CAF KISHA KUFUTWA
Taifa la Zanzibar bado lipo na husuni kwa wapenzi wa mchezo
wa soka baada ya kuojeshwa ladha ya utamu wa Shirikisho la soka Barani Afrika
(CAF) kwa siku 128 kisha juzi Ijumaa kufutwa rasmi.
Juzi Alhamis Kamati ya utendaji ya CAF ilikutana mjini Rabat,
Morocco na kuamua mambo kadhaa likiwemo hilo la Zanzibar kufutiwa uanachama
wake ambapo Viongozi wakuu wa chama cha Soka Zanzibar (ZFA) walikuwepo katika
Mkutano huo ambapo alikuwepo Rais wa ZFA Ravia Idarous Faina, Katibu Mkuu wa
ZFA Mohd Ali Hilali “Tedy” pamoja na kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Zanzibar
(Zanzibar Heroes) Hemed Suleiman “Morocco”.
Ijumaa iliyopita Rais wa Caf, Ahmad Ahman alisema Zanzibar
ilipewa nafasi hiyo kimakosa na si sahihi kwa nchi moja kuwa na wanachama
wawili wa shirikisho hilo.
Zanzibar ilipewa uanachama wakati wa utawala wa Issa Hayatou
ambaye alikuwa akiungwa mkono na TFF chini ya Jamal Malinzi, hata hivyo Hayatou
aliangushwa na Ahmad Ahmad ambaye aliibuka mshindi katika uchaguzi wa CAF.
Hata hivyo, Zanzibar kuwa sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, imefanya kuvuliwa tena uanachama huo na kuendelea kubaki kama ilivyo.
Siku 128 kuanzia siku ya Alhamis Machi 16, 2017 hadi Ijumaa July
21,2017 itaendelea kukumbukwa na Wazanzibar baada ya ZFA kuingizwa rasmi kuwa
Mwanachama wa 55 wa Shirikisho la Soka Barani Afrika “CAF” kufuatia Kikao cha
39 cha Mkutano Mkuu wa Shirikisho hilo kilichofanyika Addis Ababa nchini
Ethiopia, uanachama huo umedumu kwa siku 128 tangu siku hiyo mpaka juzi Ijumaa.
Katika kura 54 za CAF, kura 51 zimekubali Zanzibar ipatiwe
uanachama wa kudumu wa Shirikisho hilo na nchi 3 zilikataa Zanzibar isipatiwe
ambazo ni Madagascar, Benin na Seychelles ambapo Madagascar ndio nchi anayotoka
Rais wa sasa wa CAF Ahmad Ahmad.
![]() |
Wadau wa Soka wakifurahia baada ya Zanzibar kuwa mwanachama wa CAF siku hiyo kabla ya juzi kutolewa |
Comments
Post a Comment