TAIFA BADO MAPEPE, BOYS WAENDELEA KUPETA RAIS WAO
Matokeo ya ligi kuu Zanzibar 8 bora leo.
Amaan Unguja, Taifa ya Jang'ombe 0-0 Jamhuri.
Gombani Pemba, Okapi 1-2 Jang'ombe Boys.
Mabao ya Boys Khamis Mussa (Rais) dakika ya 12 na Abdi Kassim (Babi) dakika 63.
Bao la Okapi Fadhil Khamis dakika 44.
Ligi hiyo itaendelea tena Jumatatu ambapo Mwenge watacheza na Zimamoto katika uwanja wa Gombani saa10 za jioni.
Jumanne mechi nyengine 3 ambapo Okapi watasukumana na Taifa ya Jangombe katika uwanja wa Gombani saa 10 za jioni, na katika uwanja wa Amaan JKU watakipiga na Kizimbani saa 10 za jioni, kisha saa 1 usiku Jang'ombe boys dhidi ya Jamhuri.
Comments
Post a Comment