TAIFA YA JANG’OMBE KAMA SHAMBA LA BIBI, KIZIMBANI AMEJICHULIA MATUNDA YAKE, KESHO HAPATOSHI ZIMAMOTO v/s JAMHURI
![]() |
Kikosi cha Taifa ya Jang'ombe mwanzoni mwa msimu huu |
Timu ya Taifa ya Jang’ombe imekubali kufungwa mabao 3-1 nyumbani
kwao Unguja na timu ya Kizimbani kutoka Pemba katika mchezo wa ligi kuu soka ya
Zanzibar hatua ya 8 bora uliopigwa saa 1 usiku leo katika uwanja wa Amaan.
Mabao ya Kizimbani yamefungwa na Khatib Hassan dakika 11, Ali
Othman Mussa dakika ya 72 na Nassir Suleiman dakika ya 90 wakati bao pekee la
Taifa limefungwa na Ali Badru dakika 61.
Mapema hii leo Jang’ombe Boys wameichapa Mwenge 2-1 katika
uwanja wa Gombani.
RATIBA YA MECHI ZA
KESHO:-
10/7/017 Okapi vs JKU saa 10 alasiri uwanja wa Gombani
10/7/017 Zimamoto vs Jamhuri saa 10 alasiri uwanja wa Amaan
Comments
Post a Comment