TAIFA YA JANG’OMBE NA MWENGE NDIO TIMU PEKEE MICHEZO 6 YA 8 BORA HAWAJASHINDA HATA MCHEZO 1, KESHO WANAKUTANA WENYEWE SASA
Hatua ya 8 bora ya ligi kuu soka ya Zanzibar ni ligi ya
heshima tu kwaajili ya kuwatafuta Wawakilishi wa Zanzibar watakaoshiriki Mashindano
ya Kimataifa ambapo Bingwa atawakilisha kwenye Kombe la Klabu Bingwa Barani
Afrika na mshindi wa pili atawakilisha kwenye Kombe la Shirikisho Barani humo
ambapo msimu uliopita Zimamoto na KVZ waliwakilisha Zanzibar katika Mashindano
hayo.
Lakini pia timu zote 8 zilizofanikiwa kutinga hatua hiyo
zimepata fursa ya kucheza ligi kuu soka ya Zanzibar kwa msimu ujao wa mwaka
2017-2018 ambapo msimu huo ligi hiyo itakuwa na jumla ya timu 12 tu.
Yote tisa lakini kumi Timu ya Taifa ya Jang’ombe na Mwenge
haziwahi kupata ushindi hata mchezo mmoja katika michezo 6 yao yote waliyocheza
kwenye ligi hiyo nakupelekea kuwa katika nafasi ya 7 na 8 kwenye ligi hiyo.
Taifa ya Jang’ombe inashika nafasi ya 7 kwa alama zake 3
kufuatia kwenda sare 3 na kupoteza 3 ambapo mpaka sasa katika ligi hiyo hawana
furaha ya ushindi.
Mwenge nafasi ya 8 baada ya kwenda sare mchezo 1 na kupoteza
michezo 5 akiwa na alama yake 1 pekee nae anaungana na Taifa kwa kutoshinda
hata mchezo 1 kwenye ligi hiyo.
Wawili hao yani Taifa na Mwenge kesho Ijumaa wanakutana kwa pamoja kwenye Mzunguko
wa saba wa ligi hiyo mchezo ambao utapigwa saa 10 jioni katika uwanja wa Gombani huku Mashabiki
wengi wakisubiri nani ataonja furaha ya ushindi kwa mara ya kwanza au watatoka
sare na kuendeleza historia yao mbovu katika ligi hiyo ya kutoshinda hata
mchezo mmoja.
Comments
Post a Comment