VIONGOZI WA ZFA WAWILI WANAWASILI LEO SAA 4 ASUBUHI WAKITOKEA RABAT MOROCCO WALIPOPOKONYWA UANACHAMA NA CAF

Ravia Idarous Faina Rais wa ZFA (Picha ya zamani baada ya ZFA kupewa ZFA)

Rais wa Chama cha Soka Visiwani Zanzibar (ZFA) Ravia Idarous Faina pamoja na kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Zanzibar (Zanzibar Heroes) Hemed Suleiman “Morocco” wanatarajiwa kuwasili Visiwani Zanzibar saa 4:5 asubuhi ya leo Jumatatu ya July 24, 2017 kwenye uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume.

Ravia na kocha Morocco wameondoka Nairobi nchini Kenya asubuhi ya leo saa 1:35 na watatua Zanzibar asubuhi hii saa 4:05.

Katibu Mkuu wa ZFA Mohd Ali Hilali “Tedy” yeye ametua Cairo nchini Misri saa 11:40 za alfajiri ya leo, kisha leo usiku saa 5 ataondoka Cairo na atawasili Nairobi Kenya Alfajiri ya kesho saa 11 kisha ataondoka Nairobi kesho saa 1:35 za asubuhi na atawasili Zanzibar saa 4:05 za asubuhi.

Viongozi hao wa ZFA walikuwepo katika Mkutano wa Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) chini ya Kamati ya utendaji wa Shirikisho hilo ambao ulikutana mjini Rabat, Morocco na kuamua mambo kadhaa likiwemo hilo la Zanzibar kufutiwa uanachama ambapo Wazanzibar wengi pamoja na Viongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wanasubiri ripoti ya Viongozi hao ili kujulikana kwa kina mpaka Zanzibar wakavuliwa uanachama kisha Serikali watatoa taarifa rasmi baada ya kupewa ripoti hiyo na ZFA huku Serikali ikiwasisitiza Wananchi kuwa na uvumilivu na subira katika kipindi hichi.

Ijumaa iliyopita Rais wa Caf, Ahmad Ahman alisema Zanzibar ilipewa nafasi hiyo kimakosa na si sahihi kwa nchi moja kuwa na wanachama wawili wa shirikisho hilo.

Zanzibar ilipewa uanachama wakati wa utawala wa Issa Hayatou ambaye alikuwa akiungwa mkono na TFF chini ya Jamal Malinzi, hata hivyo Hayatou aliangushwa na Ahmad Ahmad ambaye aliibuka mshindi katika uchaguzi wa CAF.

Siku ya Alhamis Machi 16, 2017 itaendelea kukumbukwa na Wazanzibar baada ya ZFA kuingizwa rasmi kuwa Mwanachama wa 55 wa Shirikisho la Soka Barani Afrika “CAF” kufuatia Kikao cha 39 cha Mkutano Mkuu wa Shirikisho hilo kilichofanyika Addis Ababa nchini Ethiopia, uanachama huo umedumu kwa siku 128 tangu siku hiyo mpaka Ijumaa July 21, 2017.


Katika kura 54 za CAF, kura 51 zimekubali Zanzibar ipatiwe uanachama wa kudumu wa Shirikisho hilo na nchi 3 zilikataa Zanzibar isipatiwe ambazo ni Madagascar, Benin na Seychelles ambapo Madagascar ndio nchi anayotoka Rais wa sasa wa CAF Ahmad Ahmad.

Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

HUYU NDIYE MCHEZAJI MWENYE REKODI YA KUFUNGA MAGOLI MENGI KWENYE MECHI YA TAIFA DHIDI YA BOYS