WANAMICHEZO WAPATA SHAVU, WATEULIWA KUWA MASHEHA, MMOJA KATIBU WA WAAMUZI, MUAMUZI, MSHIKA FEDHA NA ALOKUWA KATIBU WA SQUASH
![]() |
Haji Uzia Vuai kuwa Sheha wa Shehia ya Mikarafuuni |
Jumanne iliyopita ya July 4, 2017 Mkuu wa Mkoa wa Mjini
Magharibi Ayoub Mohammed Mahmoud alifanya uteuzi wa masheha wapya wa shehia
takriban 120 za mkoa huo.
Masheha walioteuliwa siku hiyo wamo wanamichezo nguli
Visiwani Zanzibar miongoni mwao ni Mwenyekiti wa Kamati ya Waamuzi ZFA Taifa
Issa Ahmada Hijja “Jogoo” ambae ameteuliwa kuwa Sheha wa Shehia ya Mtopepo
Wilaya ya Magharibi “A” Unguja.
Mwengine ni Muamuzi wa Soka wa ZFA Taifa ambae ni Ali Haji
Ali “Mkenya” ambapo ameteuliwa kuwa Sheha wa Shehia ya Kwa Goa Wilaya ya
Magharibi “A” Unguja.
Aidha Mkuu wa Mkoa huyo pia alimteuwa mwana michezo mwengine
aliyekuwa katibu wa chama cha mpira wa Ukuta Zanzibar (Squach) ambae ni Haji
Uzia Vuai kuwa Sheha wa Shehia ya Mikarafuuni Wilaya ya Magharibi “B” Unguja.
Mwengine aliyeteuliwa kuwa Sheha ni Mshika Fedha wa ZFA
Wilaya ya Magharibi “B” Khamis Mzee Mwinshehe “Bonzo” kuwa Sheha wa Shehia ya Maungani.
Tayari viongozi hao jana wameshaapishwa mbele ya Mkuu wa Mkoa
wao ili kuzitumikia nafasi zao.
![]() |
Issa Ahmada Hijja Sheha wa Shehia ya Mtopepo |
Comments
Post a Comment