WATATU WAFUKAZANA KWA KUPACHIKA MABAO LIGI KUU YA SOKA ZANZIBAR
Mshambuliaji wa timu ya Jang’ombe Boys Khamis Mussa “Rais”,
Ahmed Ali wa Jamhuri pamoja na Mwalimu Mohd wa Jamhuri wao ndio vinara wa
kupachika mabao kwenye ligi kuu soka ya Zanzibar hatua ya 8 bora inayoendelea
katika mzunguko wake wa sita.
Washambuliaji hao mpaka sasa wameshafunga jumla ya mabao 4
kila mmoja katika michezo mitano waliyocheza.
Wengine wanaofuatia ni Ibrahim Hamad “Hilika”
wa Zimamoto, Khamis Said wa JKU, Nassor Matar wa JKU, Nabil Mohammed wa
Okapi, Seif Saleh wa Okapi, Abdull Yussuf wa Mwenge, Salim Mussa wa Mwenge,
Khatib Hassan wa Kizimbani, Nassir Suleiman wa Kizimbani, Mussa Ali wa Jamhuri
na Hassan Haji wa Zimamoto wote hao wana mabao 2.
Hakim Khamis “Men” ndie Mfungaji bora wa ligi kuu soka ya
Zanzibar msimu ulopita alifunga mabao 17 na kuisaidia timu yake Zimamoto kutwaa
ubingwa wa ligi hiyo ambapo pia aliwahi kuwa mfungaji bora wa ligi kuu soka ya
Zanzibar msimu wa mwaka 2011-2012 wakati Super Falcon ya Pemba ilitwaa ubingwa
msimu huo.
![]() |
Khamis Mussa (Rais) mshambuliaji wa J Boys |
Comments
Post a Comment