WAZANZIBAR WAZIOMBEE DUA TIMU ZAO MBILI, MJINI UNGUJA NA JKU WOTE WANACHEZA ROBO FAINALI LEO MASHINDANO YA ROLLING STONE
Na: Said Salim “Hazard” kutoka Mbulu, Manyara.
Wawakilishi wa wawili wa Zanzibar katika Mashindano ya vijana
ya Afrika Mashariki na kati ya Rolling Stone timu ya Mjini Unguja na JKU
Academy watacheza hatua ya robo fainali leo mkoa wa Manyara na Arusha ambapo
michezo yote minne ya hatua hiyo itapigwa saa 10:00 za jioni.
Kituo cha Mbulu Mkoani Manyara katika uwanja wa Julias
Nyerere kutapigwa mchezo kati ya mabingwa watetezi Wilaya ya Mjini ya Zanzibar
dhidi ya Lindi academy kutoka Lindi.
Na huko katika kituo cha Babati mkoani Manyara kutapigwa
mchezo mmoja katika uwanja wa Babati kati ya Singi Academy dhidi ya Fire boys
kutoka Karatu.
Na katika Mkoa wa Arusha kutapigwa robo fainal katika vituo
viwili tofauti katika kiwanja cha Sheikh Amry Abeid mjini humo kutapigwa mchezo
mmoja kati ya JKU academy kutoka Zanzibar dhidi ya Arusha central vijana kutoka
hapo hapo Arusha.
Na huko katika kituo cha Mererani kutakua na mchezo mwengine wa
robo fainali kati ya Saint Patrick dhidi ya Middle age.
Comments
Post a Comment