YULE MCHEZAJI WA MAFUNZO ALIYECHOMWA KISU NA KUKOSA KUCHEZA SOKA MWAKA MZIMA SASA YUPO FITI NA AMESHAANZA MAZOEZI NA WENZAKE
Mlinzi wa Kati wa timu ya Soka ya Mafunzo Kheri Salum Kheri “Chivu”
amerejea mazoezi katika kikosi chake na kuanza kujifua na wenzake baada ya
kukosa Mwaka mzima.
Beki huyo amerudi uwanjani baada ya kukaa nje msimu mzima
uliopita wa mwaka 2016-2017 ambapo alipata tatizo kufuatia kuchomwa kisu na
kijana mmoja anatuhumiwa kuwa ni muhalifu huko nyumbani kwao Migombani Mjini Unguja
ambapo tukio hilo lilitokea karibu ya mwaka sasa, na awali alianza kupatiwa
matibabu katika Hospitali ya Mnazi mmoja kisha kufanyiwa upasuaji katika Hospitali
ya Kairuki na Muhimbili huko Tanzania bara.
“Narudi uwanjani katika kipindi muhimu ambacho timu
inanihitaji kutokana na ugumu wa ligi 2, kama unavyojua sasa kuna ligi 1 na 2
na sisi Mafunzo tupo ligi 2 hivyo nataka kupigana tuipeleke Mafunzo ligi 1,
wenzangu wamenimis sana mwaka mzima lakini kwasasa namshukuru Mwenyezi Mungu
nimepoa na mazoezi nimeshaanza na wenzangu”. Alisema Kheri.
Kheri ni kaka wa damu wa Abdallah Salum Kheri (Sebo) Beki wa
Azam FC na Omar Salum Kheri “Inzaghi” mlinzi wa kushoto wa African Lyon ndugu
zake wote wakicheza soka Tanzania bara.
Comments
Post a Comment