ZANZIBAR IMEONJESHWA HARUFU YA CAF KWA SIKU 128, SASA RASMI YAVULIWA UANACHAMA
Ni taarifa mbaya kwa soka la Zanzibar baada ya kuwa
mwanachama wa 55 wa Shirikisho la Soka Barani Afrika kwa siku 128, sasa rasmi Zanzibar
imevuliwa uanachama huo.
Raisi wa Shirikisho hilo Ahmad Ahmad amesema Zanzibar
walipewa uanachama kimakosa na kama sheria zingepitiwa vizuri wasingepewa
uanachama ambapo Sababu kubwa ambayo CAF wameivua uanachama Zanzibar ni
kutokana na Visiwa hivyo kuwa ndani ya Tanzania ambao nao ni wanachama wa CAF..
“Walipewa uanachama bila kupitia vizuri kanuni ambazo ziko
wazi na zinaeleza kila kitu, kama kanuni na sheria zingepitiwa kiufasaha
wasingepewa uanachama”
“Jina la nchi linatokana na jina linaloandikwa katika umoja
wa mataifa UN na Zanzibar katika umoja huo inafahamika ipo ndani ya nchi
iitwayo Tanzania ambao ni wanachama wa CAF”. Alisema Ahmad.
Machi 16, 2017 ilikuwa ni siku nzuri na yenye historia kubwa kwa Zanzibar baada ya kuingizwa rasmi kuwa Mwanachama wa 55 wa Shirikisho la Soka Barani Afrika “CAF” kufuatia Kikao cha 39 cha Mkutano Mkuu wa Shirikisho hilo kilichofanyika Addis Ababa nchini Ethiopia lakini leo July 21, 2017 ni siku mbaya kwa Zanzibar baada ya kuvuliwa rasmi uanachama huo.
Comments
Post a Comment