ZASWA KUFANYA UHAKIKI HUKU WAKIJITAYARISHA NA UCHAGUZI, WAANDISHI WA MICHEZO WAHIMIZWA WAJIUNGE NA CHAMA HICHO
Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Zanzibar (ZASWA) kinatarajia
kufanya Uchaguzi wake wa kupata uongozi mpya uchaguzi ambao utafanyika Disemba 24,
2017.
Matayarisho hayo ya Uchaguzi tayari yameshaanza ambapo zoezi
linaloendelea sasa ni kuhakiki Wanachama na kutafuta Wanachama wapya ambapo
zoezi hilo lilianza tangu July 2, 2017 na litafikia tamati Agost 15, 2017.
Mwinyimvua Abdi Nzukwi ambae ni Mwenyekiti wa Chama hicho
amewaomba Waandishi wa Michezo wa Zanzibar kufanya uhakiki kwa wale ambao ni
wanachama na kwa Waandishi wapya wanaotaka kujiunga na chama hicho wajitokeze
kwa wingi ili wakachukue fomu za kuomba Uanachama.
“Wanachama wetu tunawaomba wajitokezee kuhakiki taarifa zao
mana tunaelekea kwenye Uchaguzi mwishoni mwa mwaka, lakini pia nawaomba
Waandishi wa michezo wapya waje kuchukua fomu kujiunga na ZASWA watapata fursa
nyingi kama ni waandishi wa michezo hapa Zanzibar, waje kuchukua fomu”.
Alisisitiza Nzukwi.
![]() |
Viongozi wa ZASWA, kushoto ni Katibu Donisya Thomas, katikati ni Mwenyekiti Mwinyimvua Abdi na kulia ni Mshika Fedha Mwajuma Juma |
Comments
Post a Comment