ZOEZI LA UHAMISHO NA USAJILI ZANZIBAR KUANZA RASMI JULY 17
Chama cha Soka Visiwani Zanzibar “ZFA” kimetangaza rasmi tarehe ya kuanza zoezi
la uhamisho na usajili kwa msimu wa mwaka 2017-2018 ambao unatarajiwa kuanza
July 17, 2017 na kumaliza Agost 17, 2017.
Katibu Mkuu wa ZFA Mohd Ali Hilaly“Tedy” amevitaka vilabu
kufata tarehe iliyowekwa ili kurahisisha zoezi hilo.
“Baada ya kupata vilabu 12 vya ligi 1 na 16 vya ligi 2 sasa tunatangaza Zoezi la uhamisho na
usajili kuanza July 17 na kumalizika Agost 17, hivyo naviomba vilabu kufuata
taratibu zilizowekwa ili kurahisisha zoezi hili”. Alisema Tedy.
Jana ZFA imepata rasmi timu 12 zitakazoshiriki ligi kuu soka
ya kwa msimu wa mwaka 2017-2018 ambapo wameamua timu zilizomaliza nafasi ya 1-6
kwa kila kanda, yani Unguja na Pemba ndizo zitakazocheza ligi kuu wakati huo
huo Bingwa atapata nafasi ya kuwakilisha Zanzibar katika Kombe la Klabu Bingwa
Barani Afrika.
Timu 16 kati ya 28 zilizosalia ambazo hazijashuka daraja
zitacheza ligi two ambapo Bingwa wa ligi hiyo atapata nafasi ya kuwakilisha
Zanzibar kwenye kombe la Shirikisho Barani Afrika.
Timu hizo 12 zilizofanikiwa kucheza ligi kuu msimu mpya wa
mwaka 2017-2018 ni JKU, Jang’ombe Boys, Zimamoto, Taifa ya Jang’ombe, Polisi,
KMKM kwa upande wa Unguja na Pemba ni Jamhuri, Kizimbani, Mwenge, Okapi,
Chipukizi na New Stars.
Kwa upande wa timu 16 zitakazocheza ligi 2 msimu mpya wa
mwaka 2017-2018 kati ya hizo 8 za Unguja na 8 za Pemba ambapo za Unguja ni
Mafunzo, KVZ, Black Sailors, Chuoni, Kilimani City, Kipanga, Miembeni City na
Charawe wakati za Pemba ni Dogomoro, Wawi Star, Shaba, Young Islander, FSC,
Hardrock, Chuo Basra na Opek.
Timu 4 za mwisho za ligi 1 zitashuka darajan la ligi 2, na
timu 4 za juu za ligi 2 zitapanda daraja la ligi 1.
![]() |
Mohd Ali Hilali-katibu wa ZFA |
Comments
Post a Comment