DALILI KUBWA JKU NA ZIMAMOTO KUWAKILISHA ZANZIBAR MASHINDANO YA CAF BAADA YA BOYS LEO KUFUNGWA NA TAIFA KUSHINDA

Timu ya Jang’ombe boys imekubali kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Okapi katika mchezo wa ligi kuu soka ya Zanzibar hatua ya 8 bora uliopigwa jioni ya leo katika uwanja wa Amaan.

Bao pekee la Okapi limefungwa na Seif Saleh dakika ya 66.

Nako huko katika uwanja wa Gombani timu ya Taifa ya Jang’ombe wakafanikiwa kuichapa Jamhuri mabao 2-0 mchezo uliopigwa leo jioni katika uwanja wa Gombani Kisiwani Pemba.

Mabao ya Taifa yote yamefungwa na Ali Badru.

Mpaka sasa JKU anaongoza akiwa na alama 24 akifuatiwa na Zimamoto mwenye points 22 huku Jamhuri akikamata nafasi ya 3 kwa alama zake 21.

Ligi hiyo itaendelea tena kesho Alhamis kati ya Kizimbani dhidi ya Taifa ya Jang'ombe katika uwanja wa Gombani ambapo  Ijumaa pia itaendelea kati ya Jamhuri dhidi ya JKU katika uwanja wa Gombani saa 10 za jioni, na katika uwanja wa Amaan Zimamoto dhidi ya Okapi.

Comments

Popular posts from this blog

WACHEZAJI WA 5 WA ZANZIBAR HEROES WAMEITWA TIMU YA TAIFA YA TANZANIA TAIFA STARS KWAAJILI YA MICHEZO MIWILI YA KIMATAIFA YA KALENDA YA FIFA.

ZANZIBAR KARIBU WATAPATA UANACHAMA WA FIFA BAADA YA KUWA MWANACHAMA WA 55 WA CAF

JKU ACADEMY HAO WATANGULIA KWENDA ARUSHA KATIKA MASHINDANO YA ROLLING STONE