HAPATOSHI KESHO AMAAN UJAMAA DHIDI YA GULIONI, MCHEZO MAALUM WA SHEREHE ZA KUTIMIZA MIAKA 60 KWA UJAMAA
Katika kusheherekea sherehe za kutimiza miaka 60 tangu
kuanzishwa timu ya Ujamaa Sports Club ya Rahaleo, kesho Jumatano majira ya saa
1 za usiku watacheza dhidi ya Gulioni FC mchezo maalum wa kirafiki katika
Uwanja wa Amaan.
Viingilio vya mchezo huo ni Shilingi 2000/=na VIP 5000/= .
Mgeni rasmi katika pambano hilo anatarajiwa kuwa mchezaji wa
zamani wa Ujamaa Sports Club ambae pia kwasasa ni Makamo wa Pili wa Rais
Zanzibar Mh Balozi Seif Ali Iddi.
Comments
Post a Comment