JKU YASHINDA 7 YAREJEA KILELENI, HUKU ZIMAMOTO NAE AKIMCHAPA MTU
Timu ya Jeshi la Kujenga Uchumi Zanzibar (JKU) imefanikiwa
kuondoka na kapu la mabao kufuatia kuichapa Kizimbani mabao 7-2 katika mchezo
wa ligi kuu soka ya Zanzibar hatua ya 8 bora uliosukumwa jioni ya leo katika
Dimba la Gombani Kisiwani Pemba.
Mabao ya JKU yamefungwa na Khamis Said dakika ya 37, 45,63 Amour
Omar dakika ya 19, Muhammed Said Mpopo dakika ya 80,90 na Issa Haidar “Mwalala”
dakika ya 89 kwa shuti kali kutoka katikati ya uwanja hadi goli, huku mabao ya kufutia machozi ya Kizimbani yote
yamefungwa na Nassir Suleiman dakika ya 50 na 73.
Mchezo mwengine leo umepigwa katika dimba la Amaan ambapo
Zimamoto wakaichapa Mwenge mabao 3-1.
Mabao ya Zimamoto yamefungwa na Ibrahim Hamad Hilika dakika
ya 12 na Nyange Othman Denge dakika ya54 na 61 ambapo bao pekee la Mwenge
limefungwa na Sharifu Hamad dakika ya 69.
Ligi hiyo itaendelea tena kesho kwa kupigwa michezo 2 katika
viwanja viwili tofauti majira ya saa 10:00 za jioni.
Katika uwanja wa Amaan watasukumana kati ya Jang’ombe boys
dhidi ya Okapi na katika uwanja wa Gombani Jamhuri watakipiga na Taifa ya Jang’ombe.
Comments
Post a Comment