KAMBI YA WANAMICHEZO MAJESHI WA TANZANIA YAENDELEA VYEMA VISIWANI ZENJ
Mashindano ya Majeshi ya Michezo ya Afrika Mashariki na Kati mwaka
huu yatafanyika Bujumbura Mjini Burundi kuanzia Agost 20, 2017 ambapo timu za Jeshi la
Wananchi wa Tanzania (JWTZ) litashiriki kwa michezo mitano ikiwemo mpira wa
Miguu, mpira wa Kikapu, mpira wa Wavu, mpira wa Pete na Riadha.
Timu hizo za JWTZ zimeweka kambi Visiwani Zanzibar ambapo
kambi hiyo inaendelea vizuri mpaka sasa huku wakipania kutwaa ubingwa.
Akizungumza na Mtandao huu Kanal Mwandike ambae ni Mkurugenzi
wa Michezo wa JWTZ amesema kambi inaendelea vizuri Zanzibar na wamepania kufanya kweli mwaka huu.
“Kambi inaendelea vizuri hapa Zanzibar na hakuna tatizo
lolote mpaka sasa, tumeshacheza michezo mbali mabli ya kirafiki na timu
zinaonesha kiwango cha hali ya juu kabisa, mwaka huu tumepania kufanya vyema
kuliko mwaka jana, mana mwaka jana tulishinda nafasi ya pili lakini mwaka huu
tutakuwa wa kwanza”. Alisema Kanal Mwandike.
Comments
Post a Comment