KOCHA WA JAMHURI MWENYE LESENI A APATA TIMU LIGI KUU BARA
Klabu ya Ruvu Shooting imemteua Abdul mutik Haji (Kiduu) kuwa
kocha mpya wa timu yao na kumpa mkataba wa mwaka mmoja, ambapo anaweza akaongezewa
miaka mengine akifanya vizuri.
Kiduu mwenye leseni A ya CAF alikuwa Kocha Mkuu wa timu ya
Jamhuri ambao ndio vinara wa ligi kuu soka ya Zanzibar na ameondoka hapo
Jamhuri baada ya kuagalia maslahi bora ziaidi Ruvu.
Akithibitisha taarifa hizo Kocha Kiduu amesema ni kweli
amejiunga na Ruvu na sasa akili yake yote ni kujipanga kuhakikisha timu yake
mpya inaleta upinzani mkubwa zaidi katika ligi kuu soka ya Tanzania bara.
“Ni kweli nipo Ruvu na nimefunga mkataba wa mwaka mmoja,
kwasasa najipanga kuhakikisha Ruvu inafanya vizuri zaidi ya msimu uliopita
katika ligi kuu bara”. Alisema Kiduu.
Kiduu amechukua nafasi ya Malale Hamsini keya ambapo pia alikuwa ni Mzanzibar kufundisha timu hiyo.
Comments
Post a Comment