MRAJIS WA MICHEZO USO KWA USO NA ZAHA, SASA WAPANGA MIKAKATI MIPYA BAADA YA KUKAA MIAKA 3 PASIPO KUCHEZWA LIGI KUU
![]() |
Suleiman Pandu Kweleza |
Mrajisi wa vyama vya michezo vya Zanzibar Suleiman Pandu
Kweleza amekutana na kamati tendaji ya muda ya chama cha Handball kwa kujadili
masuala mbali mbali ya chama hicho ikiwemo kufanya uchaguzi, kikao ambacho
kimefanyika Afis ya Mrajis iliopo Mwanakwerekwe.
Kweleza amesema lengo la kukutana na kamati tendaji ya chama
hicho cha mpira wa mikono ni kujadili vipi watafanya uchaguzi kwa kufata katiba
na maelekezo ya Baraza la Michezo Zanzibar ambapo viongozi wa mchezo huo
wamemuahidi Mrajis huyo kufanya haraka kuendesha uchaguzi huo.
“Tumekutana na kamati tendaji ya chama cha Hand Ball Zanzibar
kwa kujadili mambo mbali mbali ukiwemo uchaguzi, na viongozi hawa wameniahidi
kuharakisha kufanya uchaguzi kwa kufata katiba na maelekezo yetu kutoka baraza
la Michezo”. Alisema Kweleza.
Nae Salum Hassan ambae ni mjumbe wa kamati ya muda ya chama
cha Hand ball Zanzibar amesema chama chao ni kweli walichelewa kufanya uchaguzi
kutokana na ukata wa fedha lakini wanawashukuru Baraza kwa kuwaahidi
watawasaidia fedha za kuendesha uchaguzi huku akiahidi uchaguzi huo kufanywa
kwa haraka kutoka sasa.
“Ni kweli tulikaa muda mrefu hatujafanya uchaguzi lakini
nadhani sababu inajulikana kutokana na ukata wa fedha, lakini tunawashukuru
baraza kwa kukaa na sisi na kuona kuna umuhimu wa kutusaidia ili tufanye
uchaguzi kwa haraka, naamini uchaguzi utafanywa hivi karibuni”. Alisema Salum.
Chama cha Hand Ball Zanzibar (ZAHA) kimekumbwa na migogoro
mingi ndani ya miaka mitatu ambapo kimeshindwa hata kuendesha ligi kuu ya
Zanzibar ya Hand ball kwa muda wote huo wa miaka mitatu jambo ambalo
limepelekea kuwanyima fursa wachezaji na walimu wa mchezo huo ambao wanafanya
mazoezi lakini ligi hakuna.
Comments
Post a Comment