NUSU FAINALI MAJIMBO CUP KUANZA KESHO JUMAMOSI
Mashindano ya Majimbo ya Unguja hatua ya Nusu fainali
itapigwa kesho Jumamosi Agost 5, 2017 kati ya Jimbo la Mji Mkoongwe dhidi ya
Afisi kuu ya CCM Kisiwandui saa 10:00 za jioni katika uwanja wa Amaan.
Kwa mujibu wa mratibu wa Mashindano hayo Uledi Said amesema
mechi hiyo itakuwa bila ya kiingilio.
“Matayarisho yamekamilika mechi nusu ya kwanza itachezwa
Jumamosi nay a pili Jumapili na hakuna kiingilio”. Alisema Uledi.
Nusu fainali ya pili itapigwa Jumapili Agost 6, 2017 kati ya
Jimbo la Kwahani dhidi ya Kikwajuni saa 10:00 za jioni katika uwanja wa Amaan.
Bingwa wa Mashindano hayo atazawadiwa gari aina ya Carry.
Comments
Post a Comment