RAIS WA MASHABIKI WA MTIBWA AWATOA HOFU WENZAKE
Rais wa Mashabiki wa
Mtibwa Sugar ya Mkoani Morogoro Suleiman Nassoro “Super Cicinho” amewataka
mashabiki wenzake wasiwe na hofu na timu yao katika msimu mpya wa ligi kuu soka
Tanzania bara kwani wamepandisha wachezaji wanne wapya kutoka timu yao ndogo
wenye vipaji vya hali ya juu.
Amesema licha ya timu
yao kuondokewa na nyota kadhaa waliyokimbilia Simba na timu nyengine lakini
bado anaamini watafanya vizuri katika msimu mpya na kuleta upinzani mkubwa
kwenye ligi hiyo.
“Hatuna wasi wasi
wowote licha ya kuondoka nyota wetu ambao waliokuwa tegemeo, Mtibwa ni chuo
tumeshapandisha wachezaji wengine wanne wapya ambao wanauwezo mkubwa na
watakuwa tegemeo kwetu na Taifa kwa ujumla”.
Nyota hao wanne
waliyopandishwa ni washambuliaji Ismail Aidan na Omary Sultan pamoja na walinzi
Dickison Job na Jamal Masenga.
Agost 28, 2017 Mtibwa
Sugar wataanza kucheza mchezo wao wa kwanza wa ligi kuu soka Tanzania bara
kwenye uwanja wao wa Manungu Morogoro dhidi ya Stand United ya Shinyanga mchezo
utakaopigwa saa 10:00 za jioni.
Comments
Post a Comment