TABLE TENNIS YAPATA UONGOZI MPYA, KISANDU NDANI
Chama cha Mpira wa Meza Zanzibar “Zanzibar Table Tennis
Association (ZTTA)” kimepata viongozi wapya watakaongoza kipindi cha miaka
minne ijayo baada ya kufanyika Uchaguzi katika Ukumbi wa Baraza la Taifa la
Michezo Zanzibar (BTMZ) uliopo Mwanakwerekwe Mjini Zanzibar.
Katibu wa Kamati ya Uchaguzi Suleiman Haji (Kibabu)amewatangaza
washindi kwa nafasi saba zilizogambaniwa katika Uchaguzi huo ambapo kwa nafasi
zote wagombea walikuwa mmoja mmoja na wapiga kura walikuwa 16 hivyo kura
zilipigwa kwa ndio na hapana.
Kibabu amemtangaza Latifa Daud Jussa kuwa Mwenyekiti mpya kwenye
chama hicho baada ya kura 14 kumkubali na 2 kumkataa, nafasi ya Makamo Mwenyekiti
akashinda Faki Ali Faki baada ya kura zote 16 kumkubali, nafasi ya katibu
amejitokeza Ahmed Abdallah kashinda kwa kura 16 zote kumkubali, huku katibu msaidizi
ameshinda Omar Mohd Othman baada ya kura 16 zote kumkubali.
Wakati huo huo Mwanamama Asha Haji Ame ameshinda nafasi ya
mhasibu mkuu baada ya kupata kura 16 zote kumkubali, Abubakar Khatib Haji
(Kisandu) nae ameshinda nafasi ya Mhasibu Msaidizi baada ya kura 14 kumkubali
na kura 2 zilimkataa huku Salum Ramadhan Abdallah akishinda nafasi ya mjumbe
baada ya kura zote 16 kumkubali.
Viongozi hao wataongoza kwa muda wa miaka 4 ijayo ndipo utafanyika
uchaguzi mwengine kwa mujibu wa katiba ya Chama hicho.
![]() |
Viongozi wa Kamati ya Uchaguzi, kushoto ni Suleiman Haji (Kibabu) na kulia ni Abbas Halfan Mwenyekiti |
Comments
Post a Comment