TAIFA YA JANG’OMBE YACHEZA SIKU 2 MECHI 2 MFULULIZO LIGI KUU ZENJ
Baada ya kucheza jana Jumatano timu ya Taifa ya Jang’ombe na
kufanikiwa kuwafunga Jamhuri 2-0 katika mchezo wa ligi kuu soka ya Zanzibar
hatua ya 8 bora mchezo uliopigwa kwenye Dimba la Gombani, unaweza kushangaa na
leo Alhamis Taifa wanacheza tena mchezo mwengine wa ligi hiyo hiyo dhidi ya Kizimbani
katika uwanja wa Gombani Kisiwani
Pemba.
Mchezo huo nambari 48 ulikuwa uchezwe Jumamosi ya Agost 12,
2017 lakini Taifa wameomba wacheze tena na leo ili wawahi kurejea nyumbani
Unguja kwaajili ya kupunguza gharama wakiwepo Kisiwani huko.
“Ni kweli Taifa watacheza mechi mbili mfululizo jana na leo
kwa vile wameomba wacheze ivyo kwaajili ya kupunguza gharama ili wawahi kurudu
nyumbani Unguja kwasababu wakimaliza mchezo huu hawana tena mchezo mwengine
hapa Pemba, sasa ukiangalia ratiba mpaka Jumamosi ndo wanacheza na itabidi
wasafiri Jumapili gharama zitazidi kuwa kubwa lakini wanacheza leo Alhamis na
kesho Ijumaa wanarejea nyumbani”. Kilisema Chanzo.
Ligi kuu soka ya Zanzibar hatua hiyo ya 8 bora inachezwa kwa
visiwa viwili tofauti yani Unguja na Pemba ambapo kuna baadhi ya timu ikiwemo
Taifa wamesafiri mara mbili tofauti kwenda huko Kisiwani Pemba kucheza michezo yao
ambapo mpaka ligi hiyo inaelekea ukingoni hakuna mdhamini yoyote aliyejitokeza
jambo ambalo linawapa wakati mgumu vilabu vinavyoshiriki ligi hiyo.
Comments
Post a Comment