TANZIA-ZFA YAPATA PIGO, YAONDOKEWA NA MJUMBE WAO, MECHI YA JAMHURI NA TAIFA YALAZIMIKA KUTOCHEZWA
Chama cha Soka Visiwani Zanzibar kimepokea taarifa ya msiba
wa mjumbe wao kamati tendaji ZFA Taifa ndugu Suleiman Khamis maarufu Kamba ya
Mbuzi uliotokea asubuhi ya leo jijini Dar es salam.
Marehemu alipata nafasi hiyo ya ujumbe wa kamati tendaji
kupitia nafasi za umoja wa Vilabu kutokea Kisiwani Pemba.
Kabla ya kushika nafasi hiyo, marehemu aliwahi kuwa muamuzi
wa mpira wa miguu wakati chama cha mpira wa miguu wakati huo kikijulikana kama
EFOZA, baada ya hapo alifanikiwa kupewa nafasi ya ukatibu mkuu katika timu ya
Chipukizi ambayo kwasasa inashiriki ligi kuu soka ya Zanzibar.
Marehemu alikuwa ni kiongozi aliyesimamia haki ya kikanuni na
katiba na alikua hayupo tayari kuona haki haitendeki kwa mujibu wa taratibu za
mpira.
Taarifa kutoka kwa ndugu wa karibu ni kuwa marehemu Suleiman alikua akisumbuliwa na
Pressure na Sukari na kabla ya kusafirishwa kupelekwa Hospitali ya Agaghan
jijini Dar es salam, pia alilazwa Hospitali kuu ya Chake Chake Kisiwani Pemba.
Marehemu amezikwa leo saa 10:00 alaasiri huko kijijini kwao
Kengeja na ambapo kutokana na msiba huo ZFA wamefuta mchezo wa ligi kuu ya
Zanzibar uliokuwa uchezwe leo katika uwanja wa Gombani kati ya Jamhuri dhidi ya
Taifa ya Jang’ombe.
Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema Peponi Amiin.
![]() |
Marehemu Suleiman Khamis wa kati kati aliyevaa shati nyeupe |
Comments
Post a Comment