JKU NA MIEMBENI CITY SEPTEMBA 19 NGAO YA JAMII AMAAN
Mabingwa watetezi wa ligi
kuu soka ya Zanzibar timu ya JKU, pamoja na mabingwa wa ligi daraja la kwanza Taifa
timu ya Miembeni City watakutana Jumanne Septemba 19, mwaka huu kwenye Uwanja
wa Amaan katika mchezo wa Ngao ya Jamii kuashiria kufunguliwa kwa pazia la Ligi
Kuu soka Visiwani Zanzibar mchezo ambao utapigwa majira ya saa 10:00 za jioni.
Mjumbe wa ZFA Taifa kutoka Wilaya ya Mjini Abdul-Wahab Dau Haji ameuambia Mtandao huu kwamba, Ligi Kuu yenyewe itaanza rasmi Oktoba 3, 2017 na mchezo wa ngao utapigwa Septemba 19, 2017.
Amesema wanacheza JKU na
Miembeni City kwa kuwa ndio wenye sifa ya kucheza mchezo wa Ngao kutokana na
kufanya vyema msimu uliopita katika madaraja yao.
“Mchezo wa Ngao utachezwa
Jumanne ijayo kati ya Miembeni city na JKU, huu ni mchezo wa kufungua ligi kuu
ya Zanzibar, JKU ni Bingwa wa ligi kuu na City ni Bingwa wa daraja la kwanza
hivyo lazima wacheze wao Ngao”. Alisema Dau.
Comments
Post a Comment