KOCHA KING AJIUZULU KUIFUNDISHA KOMBAIN YA MJINI
Kocha
mkuu wa timu ya Soka ya Kombain ya Mjini Unguja Mohammed Seif “King” amejiuzulu
kuifundisha timu hiyo baada ya kupata mafanikio makubwa kwa miaka 3 mfululizo
tangu alipoanza kuifundisha kikosi hicho .
Sababu
kubwa iliyomfanya akae pembeni kocha huyo ni mafanikio makubwa aliyoyapata na
kusema kwasasa anawapa nafasi makocha wengine kuifundisha timu hiyo.
“Nawapa
nafasi makocha wenzangu kuifundiasha timu hii, nimeongoza kwa mafanikio
makubwa, kwasasa nimeamua kukaa pembeni kwani hapa Wilaya ya Mjini kuna makocha
wengi bora na wenye sifa ya kuifundisha timu hii, sasa ni fursa na wao kwao
kwani mimi nimeongoza kwa mafanikio makubwa”. Alisema King.
Kocha
King alianzaa kuifundisha timu hiyo tangu mwaka 2015 ambapo alitwaa kombe la
Wilaya za Zanzibar, mwaka 2016 akatwaa Ubingwa kwa mara ya kwanza kwenye
Mashindano ya Vijana ya Afrika Mashariki na Kati ya Rolling Stone ambapo Mjini
Unguja walishinda kombe hilo kule Arusha na mwaka huu 2017 akashinda tena kombe
hilo huko wilayani Mbulu Mkoani Manyara.
Kwasasa
Kocha huyo anafundisha timu ya Miembeni City ambayo inashiriki ligi kuu soka ya
Zanzibar kanda ya Unguja.
Comments
Post a Comment