MABINGWA WA ROLLING STONE MJINI UNGUJA WALA BATA HUKO KIZIMKAZI KWA KUJIPONGEZA
Mabingwa
wa Mashindano ya Vijana ya Afrika Mashariki na Kati ya Rolling Stone timu ya Mjini
Unguja wamepongezwa na Chama cha Soka Wilayani humo kwa kufanyiwa tafrija
maalum huko Kizimkazi Wilaya ya Kusini Unguja baada ya kuandaliwa chakula
kizuri na kupongezwa kwa wachezaji wote waliochukua kombe huko mkoani Manyara.
Wachezaji
hao walionekana wakiwa na furaha kubwa pamoja na viongozi wa ZFA Wilaya ya Mjini
akiwepo katibu mkuu Yahya Juma Ali na Mwenyekiti Hassan Haji Hamza “Chura”
pamoja na kocha mkuu Mohammed Seif “King” na msaidizi wake Ramadhan Abdulrahman “Madundo”.
Timu
hiyo ilimaliza sherehe yao hiyo kwa kucheza mechi ya kirafiki na wenyeji wao
timu ya Kizimkazi SC inayoshiriki ligi daraja la kwanza taifa na kutoa burudani
ya hali ya juu kwa watu wa Kizimkazi na kuipongezwa kwa kiwango chao kizuri
huku matokeo katika mchezo huo walienda sare ya bao 1-1.
Kikosi
cha Wachezaji 22 waliyotwaa kombe hilo huko Mbulu
ni:-
WALINDA MLANGO
Aley Ali Suleiman “Manula” (Miembeni city), Ali Mabrouk
“Al hapsy” Black Sailors na George Munish “Dida”.
WALINZI WA PEMBENI
Muharami Khamis “Terra” (Black Sailors), Abdul hamid Salum
“Ramos” (KVZ) na Hassan Chalii (Kipanga).
WALINZI WA KATI
Ali Juma Maarifa “Mabata” (Taifa ya Jang’ombe) na Abubakar Ame
“Luiz” (Membeni City).
VIUNGO WA KATI
Fahmi Salum (Mlandege), Ibrahim Chafu (Villa FC) Yakoub Amour
(Jang’ombe Boys), Mohd Ridhaa (Villa United), Talib Hamad (Kipanga), Mohd Yahya
“Banka” (Zimamoto), Seif Said “Tiote” (KVZ) na Suleiman Ali “De Jong”.
VIUNGO WA PEMBENI
Abrahman Juma “Baby” (KMKM), Mohd Jailan (Chrisc), Mohd Haji
“Box” (Jang’ombe Boys).
WASHAMBULIAJI
Ibrahim Abdallah “Imu Mkoko” (Miembeni City), Mohd Vuai “Prince”
(Miembeni City) na Abdul hamid Juma “Samatta”.
Comments
Post a Comment