MRAJIS WA MICHEZO ZANZIBAR AWATAKA ZAHA WAACHANE NA MAJUNGU
Chama cha Mpira wa Mikono Zanzibar
yani Hand ball (ZAHA) wametakiwa kuachana na majungu na badala yake kuwa na
umoja na mshikamano ili kuukuza mchezo huo.
Kauli hiyo imetolewa na Mrajis wa
Vyama vya Michezo Zanzibar, Suleiman Pandu Kweleza, ambapo pia amewasisitiza
kujitokeza kugombea nafasi mbali mbali kwenye uachaguzi wa chama hicho ambao
unatarajiwa kufanyika hivi karibuni.
Kweleza amesema umoja wao ndio
silaha ya kuukuza mchezo huo ambao unanafasi kubwa ya kuitangaza Zanzibar na
Tanzania kwa ujumla kwenye anga za Kimataifa.
“Hand ball mimi nawaomba waendelee
kuwa na umoja waache majungu mana kuna baadhi yao huwa wanalalamika, sasa
washirikiane na katika uchaguzi washiriki kugombea na si kusubiri viongozi
wapya kasha kuwapiga majungu ambayo hayana faida yoyote”. Alisema Kweleza.
Baraza la Taifa la Michezo
Zanzibar (BTMZ) kupitia Afisi ya Mrajis wa vyama vya Michezo Zanzibar bado
linaendelea na mchakato wake kwa vyama vyake vilivyokuwa havijanya Uchaguzi
vifanye haraka ambapo kwa mwaka huu tayari zaidi ya vyama 4 tayari vimeshafanya
Uchaguzi.
Vyama hivyo vilivyofanya Uchaguzi
mwaka huu ni Chama cha Mpira wa Ukuta Zanzibar “Zanzibar Squash Racket
Association (ZSRA)”, Chama cha Mpira wa Kikapu Zanzibar yani Basketball (BAZA),
Chama cha Netiboli Zanzibar (CHANEZA) na Chama cha Mpira wa Meza Zanzibar yani
Table Tennis (ZTTA) ambapo kwasasa BTMZ wapo mbioni kuhakikisha chama cha Chama
cha Hand Ball Zanzibar kinafanya uchaguzi pamoja na Chama cha Karata, Bao,
Chama cha Baskeli Zanzibar (CHABAZA) na Chama cha Riadha Zanzibar.
Comments
Post a Comment